Khartoum. Annan ayasifu mataifa fadhili kwa kuahidi kutoa ushirikiano kwa jeshi la kulinda amani la mataifa ya Afrika huko katika jimbo la Dafur.
28 Mei 2005Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Bwana Kofi Annan yuko nchini Sudan kwa ziara ya siku tatu ambayo itamchukua hadi katika jimbo lililo na machafuko la Dafur.
Hapo mapema aliuambia mkutano wa mataifa fadhili nchini Ethiopia kuwa ametiwa moyo na ahadi za kuunga mkono ujumbe wa kulinda amani wa umoja wa Afrika katika jimbo la Dafur.
Wafadhili wameahidi dola milioni 300 zaidi kwa ajili ya shughuli za kulinda amani katika jimbo hilo.
Zaidi ya watu 180,000 wamekufa katika jimbo la Dafur , na zaidi ya milioni mbili wamelazimika kuyakimbia makaazi yao. Serikali ya Sudan imekuwa mara kwa mara ikilaumiwa kwa kuzuwia upelekaji wa misaada na kuingilia shughuli za ulinzi wa amani, pamoja na kushindwa kwake kutekeleza hatua za kusitisha mapigano na kusababisha kuvunjika kwa mazungumzo ya kuleta amani mwaka jana.