Khartoum. Mwenyekiti wa AU asema hakuna haja ya majeshi kutoka nje ya Afrika.
13 Agosti 2007Matangazo
Mwenyekiti wa umoja wa Afrika , Alpha Oumar Konare, amesema kuwa wanajeshi kutoka mataifa ambayo si ya Afrika hawatahitajika kuwa sehemu ya jeshi la umoja wa mataifa na umoja wa Afrika katika jimbo la Sudan la Darfur.
Katika taarifa kufuatia mkutano na rais wa Sudan Omar al – Bashir mjini Khartoum , Konare amesema kuwa amepata ahadi nyingi za uchangiaji wa jeshi hilo kutoka mataifa ya Afrika.
Serikali ya Sudan inapinga wanajeshi kutoka nje ya bara la Afrika kushiriki katika jeshi hilo lililoimarishwa, ambalo litaundwa na wanajeshi 20,000 wa kulinda amani pamoja na maafisa 6,000 polisi.