KHARTOUM: Wanajeshi watatno wa Umoja wa Afrika wauwawa
2 Aprili 2007Matangazo
Wanajeshi watano wa kikosi cha Umoja wa Afrika cha kulinda amani katika jimbo la Darfur nchini Sudan, wameuwawa. Msemaji wa Umoja wa Afrika mjini Khartoum, Nourredine Mezni, ametangaza taarifa hiyo hii leo.
Aidha msemaji huyo amesema wanajeshi wa Umoja wa Afrika walishambuliwa na watu waliokuwa na silaha jana katika eneo la Umm Barru kaskazini magharibi mwa Darfur karibu na mpaka wa Chad.
Mzozo wa Darfur umekuwa ukiendelea kwa miaka minne na mashirika ya kimataifa yanakadiria watu takriban laki mbili wameuwawa na wengine milioni mbili unusu kulazimika kuyakimbia makazi yao.