1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KHARTOUM:Kikosi cha Umoja wa Afrika kubakia Darfur hadi mwisho wa mwaka

21 Septemba 2006
https://p.dw.com/p/CDAT

Serikali ya Sudan imeupokea uamuzi uliofanywa na Umoja wa Afrika wa kukiongezea muda hadi mwisho wa mwaka huu kikosi chake cha kulinda amani katika jimbo la mgogoro la Darfur.

Makubaliano hayo yalifikiwa kwenye mkutano wa kilele wa nchi 15 za umoja huo wanachama wa baraza la usalama na amani mjini New-York,mkutano ambao ulikwenda sambamba na mkutano wa baraza kuu la Umoja wa mataifa.

Maafisa wa Umoja wa mataifa wamethibitisha kwamba watakisaidia kwa nyenzo kikosi cha Umoja huo wa Afrika wakati majadiliano yakiendelea kuishawishi serikali ya mjini Khartoum kukubali wanajeshi wa Umoja wa mataifa kuchukua nafasi hiyo ya kulinda amani Darfur.

Rais wa Sudan Omar al- Bashir alihudhuria mkutano huo wa kilele wa Umoja wa Afrika lakini aliondoka mapema kwenye kikao hicho.