1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KHARTOUM:Sudan yaendelea na juhudi za kuwa mwenyekiti wa AU

29 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCWv

Nchi ya Sudan inathibitisha kuwa inapanga kuendelea na juhudi zake za kuwa mwenyekiti wa Umoja wa Afrika AU.Hatua hiyo inaiweka Sudan katika hali mbaya kidiplomasia kwani waangalizi vilevile viongozi wa uasi katika eneo hilo kuonya kuwa huenda juhudi za Umoja wa Afrika zikaathirika hususan katika suala la Darfur.

Umoja wa Afrika AU unakutana wiki hii nchini Ethiopia ili kutafuta mwenyekiti mpya kutoka mataifa wanachama.Umoja huo una majeshi alfu 7 wanaojaribu kutuliza ghasia katika eneo la Darfur huku waangalizi wengi wakielezea wasiwasi wao endapo Rais Bashir atapata nafasi hiyo.Kulingana na serikali ya Khartoum viongozi wa Umoja wa Afrika AU walishakubaliana katika kikao kilichopita kumchagua Bwana al Bashir.

Wakati huohuo nchi ya Chad inatisha kususia Umoja huo endapo Sudan itapata nafasi ya uwenyekiti wa Umoja wa Afrika.Hayo ni kwa mujibu wa waziri wa mashauri ya kigeni wa Chad Ahmat Allam-Mi.

Kulingana na kiongozi huyo hali katika eneo la Darfur bado ni mbaya tangu Sudan kujiondoa katika kinyanganyiro cha kuwa mwenyekiti wa uMoja wa Afrika mwaka jana.Kwa mujibu wake hali katika eneo hilo inazidi kuwa mbaya vilevile uhusiano kati ya Chad na mataifa mengine jirani aidha unazorota.