Kifaa cha mionzi kilichopotea Australia chapatikana
1 Februari 2023Matangazo
Wafanyakazi wa mamlaka inayohusika na usalama wa mionzi, wale wa kuzima moto na mashirika mengine husika, wamekipata kifaa hicho hatari kusini mwa mji wa uchimbaji madini wa Newman, baada ya kukitafuta kwa mamia ya kilomita katika eneo hilo lenye wakaazi wachache.
Stephen Dawson, waziri wa huduma za dharura magharibi mwa Australia, amesema kupatikana kwa kifaa hicho ni jambo la kipekee sana.
Taarifa zinasema kimepatikana ndani ya magunia ya nyasi.
Kupotea kwa kifaa hicho chenye mionzi hatari mapema mwezi wa Januari kulizusha wasiwasi.
Kampuni ya uchimbaji madini, Rio Tinto, imeomba radhi kwa kisa hicho na imesema imelishirikisha shirika jingine lenye utaalamu zaidi kuweza kukishughulikia na kukisafirisha kunakohitajika.