Kifo cha Morgan Tsvangirai ni mshtuko na huzuni
15 Februari 2018Kiongozi maarufu wa upinzani wa Zimbabwe Morgan Tsvangirai amefariki dunia. Tsvangirai aliyekuwa kiongozi wa chama cha Movement for Democratic Change (MDC) alifariki jana Jumatano baada ya kusumbuliwa kwa muda mrefu na maradhi ya saratani ya utumbo. Alifariki akiwa na umri wa miaka 65 huko nchini Afrika Kusini alikokuwa anatibiwa.
Kifo cha Morgan Tvangirai kimepokelewa kwa mshtuko na huzuni kubwa. Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta na serikali ya Botswana wametoa rambirambi zao. Naibu katibu mkuu wa chama cha ANC nchini Afrika Kusini Jesse Duarte amesema chama chake kimepokea habari za kifo cha kiongozi huyo wa chama cha MDC bwana Morgan Tsvangirai kwa huzuni kubwa.
Bi Duarte amesema chama cha ANC kinatoa rambirambi zake kwa familia ya Bw Tsvangirai na wafuasi wote wa chama cha MDC. Wazimbawe wamesema kifo cha kiongozi huyo wa upinzani ni hasara kubwa kwa taifa kma anavyoeleza bwana Robson Musarafu.
Mwanasiasa huyo maarufu zaidi wa Zimbabwe na aliyekuwa kiongozi wa vyama vya wafanyakazi katika sekta ya migodi Morgan Tsvangirai amekimekiwacha chama chake cha MDC ndani ya hali isiyoeleweka miezi mitatu baada ya jeshi nchini Zimbabwe kumng'oa madarakani kiongozi wa muda mrefu, Robert Mugabe, huku uchaguzi nchini Zimbabwe ukiwa unafanyika ndani ya miezi sita ijayo.
Mwandishi: Zainab Aziz/RTRE/AFPE
Mhariri: Josephat Charo