Kifungo cha tabibu chaikera Marekani
25 Mei 2012Hatua hiyo Marekani imeanza kwaBaraza la Seneti kupungua msaada wa dola za Kimerekani milioni 33 ambazo zilikuwa msaada mkubwa kwa Pakistan ambayo imo katika mapigano kwa muda sasa. Hiyo inaamanisha kuwa sawa na makato ya dola milioni moja kila mwaka ambapo daktari Shakir Afridi atakuwa gerezani.
Richard Durbin ambaye ni miongoni mwa maseneta wa taifa hilo amesema kitendo cha uamuzi huo wa kupunguza msaada, ulioungwa mkono kwa kura 30 na hakukuwa na kura hata moja iliyopinga, kinaonyesha namna walivyochukizwa na kifungo kwa dakitari huyo.
Seneta Durbin ambaye ni senata nambari mbili kutoka chama cha Demokratiki, chama cha Rais Barack Obama ameongeza kuwa kitendo cha Pakistan kusema kuwa tabibu huyo ni msaliti kwa kufanikisha kupatikana kwa Osama bin Laden ni dhihaka kubwa kwa Marekani.
Uamuzi wa kamati hiyo ya matumizi umefikia maamuzi haya baada ya kamati ndogo kuitadhalisha Pakistan kuwa Marekani inaweza kupunguza misaada kwa taifa hilo ikiwa halitafungua njia kwa majeshi ya NATO katika nchi jirani na Afghanistan.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Hillay Clinton alisema hakukuwa na sababu za msingi kwa Pakistan Kumfunga Daktari Afridi na kaapa Marekani itahakisha suala hili kuigharimu Pakistan.
" Marekani haikubaliani na misingi ya hukumu hii ya Dakitari Afridi kwani msaada wake ulikuwa mkubwa kwa kupatikana kwa muhalifu mkubwa duniani."
Dakitari Shafidi alituhumiwa kwa kutoa chanjo za uongo katika kampeni ya chanjo ambayo ilisaidia kupata taarifa za kinasaba kumhusu Osama Bin Laden na familia yake na inaaminika ziliisaidia mno idara ya upelelezi ya Marekani FBI na ile ya ujasusi CIA , kujua mahala alipo Osama Bin Laden.
Kiongozi huyo wa zamani wa Al-Qaeda aliuwawa katika mji wa Abbottabad mwaka mmoja uliopita na kikosi maalumu cha Marekani. Tangu kulipotokea tukio hilo kumekuwa na shutuma nyingi kwa Pakistan kutoka Marekani. Huku baadhi ya Wamarekani wakilitaka taifa lao kuinyima misaada nchi hiyo.
Kwa muda sasa Pakistan imekuwa miongoni mwa mataifa yanayopokea msaada mkubwa kutoka Marekani .
Mwandishi:Adeladius Makwega, RTRE
Mhariri: Abdul-Rahman