JamiiTunisia
Mamlaka nchini Tunisia yawaokoa wahamiaji 34
16 Machi 2024Matangazo
Taarifa ya Walinzi wa Kitaifa imesema kuna uwezekano kwamba watu wengine 34 wamepotea, baada ya manusura kuwaarifu kwamba kulikuwa boti waliyoipanda ilikuwa imewabeba watu 70 kabla ya kupinduka.
Walinzi hao wamesema bado wanawatafuta watu waliopotea.
Tunisia na Libya zimekuwa zikitumiwa kwa kiasi kikubwa na wahamiaji wanaoondoka Afrika, ambao hupita njia hatari ya bahari wakikimbilia Ulaya kutafuta maisha bora kila mwaka .
Shirika la Kimataifa la Uhamiaji, IOM limesema watu 2,498 walikufa au kupotea walipokuwa wakijaribu kuvuka bahari ya Mediterania mwaka uliopita, ikiwa ni ongezeko la asilimia 75 ikilinganishwa na mwaka 2022.