SiasaAsia
Kim Jong Un akutana na waziri wa ulinzi wa Urusi
27 Julai 2023Matangazo
Mjumbe huyo wa Rais Vladimir Putin amekutana na kiongozi wa Korea Kaskazini wakati ambapo nchi hiyo iliyojitenga na mataifa mengine ulimwenguni ikiadhimisha miaka 70 tangu vita vya Korea vya kati ya mwaka 1950-1953 vilipositishwa.
Katika mkutano huo, Shoigu anaripotiwa kumuwasilishia Kim barua "nzuri" iliyotiwa saini na Rais Vladimir Putin.
Soma zaidi: Kim Jong Un akutana na ujumbe wa China
Hata hivyo, haikuwekwa wazi masuala ya kijeshi yaliyojadiliwa katika mkutano wa viongozi hao wawili.
Korea Kaskazini imekuwa ikiiunga mkono Urusi katika vita vyake na Ukraine ikisema nchi za Magharibi zinazoongozwa na Marekani, ndizo zilizoipelekea Urusi kuchukua hatua za kulinda maslahi yake ya kiusalama.