Kim Jong Un atishia kutumia nyuklia
4 Oktoba 2024Haya ni kulingana na taarifa iliyotolewa na vyombo vya habari nchini humo.
Hii ni baada ya kiongozi wa Korea Kusini kuuonya utawala wa Kim kwamba utaangushwa iwapo atathubutu kutumia zana za nyuklia.
Kim ametoa kauli hiyo wakati alipofanya ziara katika kitengo cha operesheni maalum cha jeshi.
Soma zaidi: Kim atishia kuisambaratisha Korea Kusini kwa nyuklia
Majibizano kama hayo baina ya mataifa hayo mawili si jambo geni ila yanafanyika wakati ambapo kuna uhasama mkubwa baina ya mataifa hayo kutokana na hatua ya Korea Kaskazini hivi majuzi kufichua kwamba ina kinu cha nyuklia na hatua yake ya kuendelea kufanyia majaribio makombora.
Wachambuzi wanasema wiki ijayo, bunge la Korea Kaskazini linatarajiwa kupitisha na kutangaza rasmi uhasama baina ya mataifa hayo mawili katika Rasi ya Korea, hatua itakayokuwa kiashiria rasmi cha kukataa maridhiano na Korea Kusini na kuweka mipaka mipya ya mataifa hayo.