1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaKorea Kaskazini

Kim na Putin watakiana ushindi dhidi ya ''mabeberu''

12 Oktoba 2023

Kim na Putin kuendeleza mahusiano yao na kutakiana ushindi dhidi ya "utawala wa upande mmoja na shinikizo la mabeberu."

https://p.dw.com/p/4XRBs
Kim amemuambia Putin kuwa ameridhishwa na mazungumzo ya kina baina yao.
Kim amemuambia Putin kuwa ameridhishwa na mazungumzo ya kina baina yao.Picha: RUSSIAN ENVIRONMENT MINISTRY/AFP

Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un, na Rais Vladimir Putin wa Urusi wameandikiana barua hivi  kila mmoja akiapa kuendeleza mahusiano yao na kutakiana ushindi kwenye kile walichokiita "utawala wa upande mmoja na shinikizo la mabeberu."

Kwa mujibu wa shirika la habari la Korea Kaskazini, KCNA, Kim amemuambia Putin kuwa ameridhishwa na mazungumzo ya kina baina yao, wakati kiongozi huyo alipoitembelea Moscow mwezi mmoja uliopita, ambapo wawili hao walijadiliana masuala ya ushirikiano wa kijeshi na vita nchini Ukraine.

Kwa upande wake, Putin ameamuambia Kim kwenye barua yake kuwa ana uhakika watashirikiana kujenga mataifa imara kwa maslahi ya watu wao na utulivu wa kanda nzima ya kaskazini mashariki mwa Asia.

Zikiwa zimetengwa na mataifa ya Magharibi, Urusi na Korea Kaskazini zimekuwa marafiki wakubwa wanaojinasibisha na upinzani dhidi ya wale wanaowaita "mabeberu wa ulimwengu."