1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kimbunga chauwa zaidi ya watu 70 Marekani

11 Desemba 2021

Kimbunga Tornado kilicho tawanyika na kuyakumba maeneo ya majimbo sita tofauti nchini Marekani kimesababisha watu zaidi ya 70 kupoteza maisha.

https://p.dw.com/p/448zJ
USA Kentucky Tornado
Picha: Dylan T. Lovan/AP/picture alliance

Akithibitisha athari hiyo Gavana wa jimbo la Kentucky amesema pamoja na vifo vya idadi hiyo ya watu wanaopindukia 70 upo uwezekano wa idadi hiyo kuongezeka zaidi. Amesema kimbuka hicho pia kimefanya uharibfu mkubwa wa makazi.

Gavana Andy Beshear amesema tatizo hilo limelikumba eneo la umbali wa maili 20 kwa Kentucky pekee na idadi ya vifo inaweza kuzidi 100 kwa rekodi za majimbo mengine 10 zaidi.

Viwanda kadhaa vimeathirika vibaya katika maeneo tofauti.

USA Kentucky Frankfort Andy Beshear
Gavana wa jimbo la Kentacky Andy BeshearPicha: VNRP/EBU

Akizungumza na waandishi wa habari Jumamosi gavana hiyo amesema kimbunga hicho, tonardo, kimeingia katika rekodi ya kuwa chenye uharibifu zaidi. Kimbunga kimekikumba kiwanda cha mishumaa cha Kentucky, eneo la kampuni ya Amazon jimboni Illios na nyumba ya wazee ya Arkansas.

Gavana Beshear aliongeza kwa kusema takribani watu 110 walikuwa katika moja ya kiwanda cha jimbo hilo wakati kimbunga hicho kilipozuka. Awali Asubuhi maafisa walithibitisha kutoka vifo vya watu 18, lakini baadae Beshear alisema idadi ya vifo inaweuza kuwa imeongezeka.

USA -Tornado in Illinois
Ghala la kampuni ya vifurushi ya AmazonPicha: Michael Thomas/Getty Images

Polisi ya jimbo la Kentucky imesema vikosi vya uokozi vimekuwa vikitumia vifaa vya hali ya juu katika kuondoa vifusi katika kiwanda cha mishumaa kilichopo magharibi mwa jimbo hilo. Kwa wakati huo ilielezwa miili ya watu kadhaa iliopolewa katika vifusi inagwa ilishindikana kufahamika ikdadi yao.

Rais Joe Biden atoa ahadi ya hali na mali katika kuwasaidia wahanga.

Biden
Rais Joe Biden wa MarekaniPicha: picture alliance / ASSOCIATED PRESS

Katika ukurasa wake wa Twitter Rais Joe Biden aliandika kwamba amepewa taarifa ya athari za kimbunga hicho na kutoa ahadi ya kufanya kila linalohitajika katika maeneo yaliathirika katika jitihada ya kuwasaka wahanga na tathimini ya athari pia itaendelea.

Manusura mmoja Kyana Parsons-Perez, aliyekuwa mfanya kazi wa kiwanda kilichoporomoka alinaswa na kuzuiwa na mapande ya zege kwa takribani masaa mawili kabla ya kuokolewa. Katika mahojiano na kituo kimoja cha televisheni nchini Marekani alisema hakuweza kujua kama angeweza kunusurika.

Amesema kabla yakimbunga kulikumba jengo hilo jengo lilianza kutetemeka, alianza kusikia mizizimo ya upepo mkali, hata hivyo hakujua kama angeweza kunusurika na kuwa hai hadi wakati huu.

Miongoni mwa walishiriki jitihada ya uokozi walikuwa wafungwa wa gereza la Graves. Manusura Kyana Parsons-Perez amesema wangeweza kutoroka kwa uhuru walioupata lakini hakufanya hivyo na badala yake walishiriki kwa hali na mali katika jitihada za uokozi.

Chanzo: AP