JamiiMsumbiji
Kimbunga Freddy kupiga tena Msumbiji
10 Machi 2023Matangazo
Shirika la kukabiliana na majanga la Msumbiji limesema kuwa zaidi ya watu 166,000 waliathiriwa wakati kimbunga hicho kilipoikumba kusini mwa Msumbiji wiki mbili zilizopita, na mafuriko kuharibu barabara, nyumba na shule.
Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayoratibu masuala ya kiutu, OCHA, imesema watu wapatao 565,000 wako katika hatari katika majimbo ya Zambezia, tete, Sofala na Nampula, huku jimbo la Zambezia likitarajiwa kuathiriwa zaidi.
Kimbunga Freddy kitasababisha mvua kubwa Msumbiji pamoja na kusini mwa Malawi. Shirika la Hali ya Hewa Duniani, WMO limesema huenda likaanzisha uchunguzi baada ya kimbunga hicho kutoweka, ili kubaini iwapo kilivunja rekodi hiyo kwa muda mrefu zaidi.