1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kimbunga Milton chaongezeka kasi kuelekea Mexico

7 Oktoba 2024

Kasi ya kimbunga Milton imeendelea kuongezeka leo Jumatatu, huku kukiwa na utabiri wa upepo mkali na dhoruba zitakazosababisha mawimbi katika rasi ya Yucatan ya Mexico.

https://p.dw.com/p/4lVfD
Marekani, North Carolina 2024 | Athari za Kimbunga Helene
Kimbunga Helene kimeathiri miundombinu nchini Marekani siku chache kabla ya kimbunga kingine cha Militon kuvamia nchini MexicoPicha: Jonathan Drake/REUTERS

Kimbunga hicho cha Milton kinafuatana na kimbunga hatari cha Helene ambacho kilipiga maeneo hayo hayo, na baadhi ya wakazi wa Florida wameamriwa kuyahama tena makazi yao.

Wafanyakazi wa huduma za dharura bado wanaendela kutaoa misaada kwa wahanga wa kimbunga Helene ambayo iliua zaidi ya watu 225 katika majimbo kadhaa kusini mashariki mwa Marekani.

Kasi ya kimbunga hicho Milton inaongezeka kabla ya kuufikia mji wa Florida nchini Marekani siku ya Jumatano.

Gavana wa Florida Ron DeSantis ametangaza kaunti 51 kati ya 67 za jimbo hilo kuwa ziko katika hali ya hatari kutokana na Kimbunga Milton, akitabiri dhoruba hiyo inaweza kuwa na "athari kubwa zaidi."