KINSHASA: Ban Ki Moon ziarani Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo
27 Januari 2007Matangazo
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon ametoa mwito kwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo kuhifadhi haki za binadamu na kurejesha mamlaka ya kisiasa kwani hayo ni muhimu kwa amani na demokrasia nchini.Katibu Mkuu Ban,alikuwa akizungumza mbele ya bunge jipya la Kongo ambalo lilichaguliwa mwaka 2006.Ban vile vile alitembelea vikosi vya amani vya Umoja wa Mataifa vilivyokuwepo nchini Kongo.Tume hiyo ya Umoja wa Mataifa ya takriban wanajeshi 18,000 ni kubwa kabisa kote duniani.Katibu Mkuu Ban ameahidi kuwa bara la Afrika litaendelea kupewa umuhimu mkubwa katika ajenda ya Umoja wa Mataifa.