Ayatollah: Kundi la Hezbollah la Lebanon halitasambaratika
25 Septemba 2024Kiongozi mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei amesema leo kuwa kuuliwa kwa makamanda wa Hezbollah hakutalisambaratisha kundi hilo baada ya Israel kuwalenga viongozi wakuu wa kundi hilo linaloungwa mkono na Iran wakati wa mashambulizi mabaya ya anga nchini Lebanon. Baraza la Usalama la UN laijadili hali ya Mashariki ya Kati
Ushindi ni wa Hezbollah kufikia sasa. Sababu ni mauaji ya watu. Ikiwa utawala wa Kizayuni ungeweza kuwashinda wanamgambo wa Gaza au Lebanon au Ukingo wa Magharibi, usingehitajika kuonyesha sura yake mbaya duniani na kufanya uhalifu huu dhidi ya makazi, hospitali, shule, wanawake na watoto.
Khamenei pia ameilaumu Marekani kwa ongezeko la mapigano nchini Lebanon, yanayofuata mashambulizi ya wiki iliyopita yaliolipua vifaa vya mawasiliano vilivyosambazwa na Hezbollah na kusema licha ya madai ya Marekani kwamba haikufahamu mapema mipango hiyo ya Israel, inafahamu, inahusika na inataka ushindi wa uongozi wa Kizayuni.