1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kiongozi wa Greenland akutana na Mfalme wa Denmark

8 Januari 2025

Waziri Mkuu wa Greeland Mute Egede amekutana leo na mfalme Frederik wa Denmark, baada ya Rais mteule wa Marekani Donald Trump kusema anataka kuchukua udhibiti wa kisiwa hicho cha Bahari ya Arctic.

https://p.dw.com/p/4oxGM
Waziri Mkuu wa Greenland Mute Egede
Waziri Mkuu wa Greenland Mute EgedePicha: LEIFF JOSEFSEN/Ritzau Scanpix/AFP/Getty Images

Waziri Mkuu wa Greeland Mute Egede amekutana leo na mfalme Frederik wa Denmark, baada ya Rais mteule wa Marekani Donald Trump kusema anataka kuchukua udhibiti wa kisiwa hicho cha Bahari ya Arctic.

Katika mazungumzo hayo, Waziri wa Mambo ya nje wa Denmark Lars Lokke Rasmussen amesema Greenland inaweza kujitegemea ikiwa wakaazi wake watataka lakini haiwezi kuwa jimbo la Marekani.

Soma pia: Kauli za Trump zakemewa vikali na viongozi duniani

Waziri Mkuu wa Greenland Mute Egede, ambaye ni kiongozi wa chama cha kisiasa cha mrengo wa kushoto kinachounga mkono uhuru wa mkoa huo kutoka kwa Greenland, aliwasili tangu jana mjini Copenhagen katika ziara iliyopangwa.

Greenland ina idadi ya wakaazi 57,000. Denmark inawajibika kwa usalama na ulinzi wa Greenland, lakini uwezo wake wa kijeshi huko ni meli nne pekee za ukaguzi, ndege ya moja uchunguzi aina ya Challenger, na doria zinazofanywa na mbwa wanaoishi kwenye mazingira ya theluji kali.