SiasaKorea Kaskazini
Kim Jong Un atoa wito wa maandalizi ya haraka ya vita
28 Desemba 2023Matangazo
Kim amesema hayo kwenye mkutano wa sherehe za mwisho wa mwaka wa chama hicho ambapo pia anatarajiwa kutangaza maamuzi muhimu ya sera kwa mwaka 2024.
Soma pia;Kim Jong Un asifu mafanikio ya Korea Kaskazini mwaka 2023
Matamshi hayo yanakuja wiki moja tu baada ya Kim kuonya kwamba nchi yake haitasita kufanya shambulio la nyuklia ikiwa "itachokozwa " kwa silaha za nyuklia.
Soma pia:Korea Kaskazini yalitaka jeshi lake liwe tayari kujibu uchokozi
Korea Kusini, Japan na Marekani zimeongeza ushirikiano wa ulinzi wakati ambapo Korea Kaskazini imefanya mfululizo wa majaribio ya silaha za nyuklia mwaka huu, na hivi karibuni zimeanzisha mfumo wa kupata data za wakati halisi kuhusu hatua za Kaskazini za kurusha makombora.