1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaBangladesh

Kiongozi wa mpito wa Bangladesh atoa rai ya utulivu

7 Agosti 2024

Mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel Muhammad Yunus, aliyechaguliwa kuwa kiongozi wa serikali ya mpito ya Bangladesh baada ya Waziri Mkuu wa nchi hiyo Sheikh Hasina kuondoka madarakani amewataka Wabangladesh wawe watulivu.

https://p.dw.com/p/4jDL6
Kiongozi wa mpito wa Bangladesh Muhammad Yunus
Kiongozi wa mpito wa Bangladesh Muhammad Yunus.Picha: Raphael Lafargue/abaca/picture alliance

Pia amewarai waitumie fursa iliyopo ili kulijenga taifa bora. Amewasihi watu wote wajieupushe na vitendo vyovyote vya matumizi ya nguvu.

Yunus ametoa kauli hiyo siku moja kabla ya kurejea nchini Bangladesh kutoka Ulaya.

Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 84 ataiongoza serikali ya mpito baada ya kufanyika maandamano yaliyomlazimisha Waziri Mkuu Hasina kuikimbia nchi. Yunus pia amesema ataitisha uchaguzi katika miezi michache ijayo.