1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kiongozi wa upinzani Shah Mahmood Qureshi akamatwa Pakistan

20 Agosti 2023

Shirika la upelelezi la Pakistan limemkamata kiongozi wa upinzani, ambaye ni mshirika wa karibu wa Waziri Mkuu wa Zamani aliyehukumiwa Imran Khan.

https://p.dw.com/p/4VMxa
Vor dem Misstrauensvotum in Pakistan - Shah Mahmood Qureshi
Picha: Anjum Naveed/AP/dpa/picture alliance

Taasisi hiyo imesema imemkamata Shah Mahmood Qureshi kwa kutoa siri za serikali na kuhujumu maslahi ya nchi. Qureshi alikamatwa jana usiku nyumbani kwake kwa kufichua barua mwaka uliyopita iliyodai kwamba Khan aliondolewa madarakani na Marekani.

Barua hiyo haijaonekana hadharani lakini inasemekana yalikuwa mawasiliano ya kidiplomasia kati ya balozi wa Pakistan nchini Marekani na wizara ya mambo ya kigeni ya Pakistan. 

Mawakili wa Imran Khan kukutana naye baada ya hukumu ya jela

Kamata kamata inadaiwa kuwa muendelezo wa mvutano uliopo kati ya serikali ya Waziri Mkuu anaeondoka Shehbaz Sharif na mtangulizi wake Khan aliyefungwa jela mapema mwezi huu kwa makosa ya ufisadi.