Machar awasili Sudan Kusini kukutana na Kiir
19 Oktoba 2019Katika ziara yake hiyo ya siku mbili, Machar atakutana pia na Balozi wa Mareani katika Umoja wa Mataifa, ambaye atawasili kesho Jumapili na ujumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Ujumbe huo unatarajiwa kuhimiza makubaliano hayo ya amani yaliyosainiwa mwaka uliopita kusonga mbele baada ya ucheleweshaji wa mara kwa mara. Vita vya wenyewe kwa wenyewe vya miaka miaka mitano, vimesababisha vifo vya vya karibu watu 400,000 na mamilioni wengine kupoteza maisha yao.
Upinzani umesema Machar hatorudi nyumbani kuunda serikali ifikapo tarehe iliyopangwa ya Novemba 12, isipokuwa kuweko na mpangilio madhubuti wa usalama. Kabla Machar kurudi jeshi la pamoja la wanajeshi 41,500 wa upinzani na wa serikali linalazimika kutayarishwa pamoja na kikosi cha ulinzi cha pamoja cha wanajeshi 3,000 kulinda watu muhimu. Lakini hadi sasa kuna wanajeshi 1,000 wa kikosi hicho cha pamoja na mipangilio ya usalama haitoweza haitokamilishwa ifikapo tarehe ya mwisho, naibu msemaji wa upinzaji Manawa Peter Gatkuoth alisema.
Marekani imeonya kuwa itatafakari tena uhusiano wake na Sudan Kusini iwapo serikali haitaunda serikali siku iliyoahidiwa.
Mara ya mwisho kwa viongozi hao kukutana na kwa ana ni mwezi Septemba, walipojadili masuala muhimu kuhusu makubaliano hayo dhaifu ya kutafuta amani. Mkutano huo kati ya Machar na Kiir ulilenga kuharakisha mchakato wa uchunguzi wa usalama na kuungana tena kwa vikosi vyao, lakini pande hizo mbili ziliondoka kwenye mazungumzo na maoni tofauti bila ya muafaka.