1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSenegal

Ousmane Sonko arejeshwa gerezani baada ya matibabu

15 Novemba 2023

Kiongozi wa upinzani wa Senegal Ousmane Sonko amerejeshwa gerezani baada ya wiki kadhaa za kupewa matibabu hospitalini, kufuatia mgomo wake wa kula, kupinga kifungo chake kwa mashitaka anayosema yalichochewa kisiasa

https://p.dw.com/p/4Yqy7
Ousmane Sonko
Kiongozi wa upinzani Senegal Ousmane SonkoPicha: Cooper Inveen/REUTERS

Tangazo la Sonko kurejeshwa jela limejiri siku chache tu kabla ya Mahakama ya Juu ya Senegal kufanya uamuzi wa kama mwanasiasa huyo anaweza kushiriki katika uchaguzi ujao wa Februari licha ya kuondolewa kwenye orodha ya uchaguzi wa nchi hiyo baada ya kutiwa hatiani kwa mashitaka ya rushwa mapema mwaka huu.

Maafisa wa idara ya magereza wamesema kuhamishwa kwa Sonko katika gereza la Cap Manuel mjini Dakar jana kulifanyika kutokana na mapendekezo ya daktari anayemhudumia.

Mwanasiasa wa upinzani wa Senegal Ousmane Sonko akamatwa

Sonko alimaliza katika nafasi ya tatu katika uchaguzi uliopita wa rais, na wafuasi wake wanaamini kuwa msururu wa tuhuma za uhalifu zilizofunguliwa dhidi yake tangu mwaka wa 2021 ni sehemu ya kampeni ya kuivunja mipango yake ya kisiasa kabla ya uchaguzi wa rais Februari mwakani.