Kiongozi wa upinzani Tanzania ataka katiba mpya
12 Aprili 2021Mbowe, mwenyekiti wa chama kikubwa cha upinzani,Chadema kupitia hotuba yake hiyo iliyogusia hali ya taifa,alisema katiba ya sasa inampa mtu nafasi ya kuwa Dikteta au mfalme na kwahivyo serikali inapaswa kulipa kipaumbele suala la kuweka ratiba ya kufanyika mchakato wa kuibadili katiba.
Som pia: Uganda Tanzania zasaini mkataba wa bomba la mafuta
Kadhalika kiongozi huyo wa upinzani nchini Tanzania amemtolea mwito rais wa sasa Samia Suluhu Hassan kuharakisha pendekezo lake lililowasilishwa Jumanne wiki iliyopita la kuunda kamati ya kitaalamu ya wanasayansi ya kufanya utafiti juu ya ugonjwa wa Covid-19.
Mbowe ametoa wito wa kuwepo maridhiano kulirejesha taifa hilo katika kile alichokiita mkondo wa kidemokrasia.
Je hilo linawezekana? Zaidi Amina Abubakar amezungumza na Pasco Mayala mwaandishi habari na mchambuzi wa kisiasa nchini Tanzania.Sikiliza mahojiano.