Nadia Abeid binti wa miaka 22 kutoka Mombasa, pwani ya Kenya anatumia kipaji chake cha kufuma kwa kutumia uzi na sindano tu kujitafutia riziki. Nadia anatengeneza bidhaa mbalimbali kama vile sweta, skafu, mabegi, mapambo ya kuta, maua ya kisanii, pini za nywele na mito miongoni mwa bidhaa nyingine. Amejifunza ujuzi huo kwa kutazama vidio kupitia mtandao wa YouTube na sasa anafundisha wenzake.