Kipchoge apasha misuli moto kwa ushindi Enschede
19 Aprili 2021Matangazo
Eliud Kipchoge, bingwa mtetezi wa Olimpiki na anayeshirikilia rekodi ya dunia, ameshinda Jumapili mbio za marathon ya Enschede ikiwa ni sehemu ya kupasha misuli moto tayari kwa michezo ya Olimpiki ya Tokyo.
Mkenya huyo mwenye umri wa miaka 36 alikamilisha mbio hizo, za mizunguko nane katika uwanja wa ndege wa Enschede, akitumia muda wa saa 2 dakika 4 na sekunde 30.
Hafla hiyo iliyowashirikisha wanariadha walioalikwa pekee, ambayo ilitumika kama mbio za kufuzu katika Michezo ya Tokyo, awali ilipangwa kufanyika Hamburg, Ujerumani lakini ikahamishiwa Uholanzi na kwa sababu ya janga la corona.
AFP/DPA/AP/Reuters