1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kiptum atahadharishwa baada ya kuvunja rekodi ya dunia

9 Oktoba 2023

Kocha wa mwanariadha wa Kenya anayeshikilia rekodi ya dunia ya Marathon Kelvin Kiptum anasema nyota huyo hatoacha kufanya mazoezi makali, ingawa huenda hatua hiyo ikafupisha taaluma yake.

https://p.dw.com/p/4XJBu
USA Chicago | Marathon - Rekodi ya Dunia - Mshindi - Kelvin Kiptum
Kelvin KiptumPicha: KAMIL KRZACZYNSKI/AFP/Getty Images

Kiptum mwenye umri wa miaka 23 aliweka rekodi ya dunia hapo Jumapili kwa kuandikisha muda wa saa 2 na sekunde 35 katika mbio za marathon za Chicago. Ushindi huo wa Jumapili ulikuwa wa tatu kwake katika marathon tatu alizokimbia baada ya kupata ushindi katika marathon za Valencia na London pia.

Na sasa kocha wa Gervais Hakizimana anasema Kiptum anafanya mazoezi makali mno kwa muda mrefu na anakabiliwa na hatari ya kupata majeraha ila mwenyewe hataki kupunguza kasi ya mazoezi.

USA Chicago | Marathon - Rekodi ya Dunia - Mshindi - Kelvin Kiptum
Kelvin Kiptum baada ya kumaliza marathon ya ChicagoPicha: KAMIL KRZACZYNSKI/AFP/Getty Images

Hazimana anasema iwapo hatopunguza kasi yake ya mazoezi basi baada ya miaka mitano huenda taaluma yake ikawa imefikia kikomo.

"Nilitazama muda mbele yangu nikajiambia wacha nijaribu kukimbia chini ya saa mbili ila kwa bahati mbaya haikuwezekana," alisema Kiptum.

Sifan Hassan kutoka Uholanzi ndiye aliyekuwa mshindi upande wa kina dada alipotimka kwa saa 2 dakika 13 na sekunde 44 huo ukiwa ni muda wa pili wa kasi zaidi duniani baada ya ile rekodi ya dunia iliyowekwa na Tigst Assefa wa Ethiopia katika marathon ya Berlin.