Kisa cha kwanza cha COVID-19 chagundulika Rohingya
15 Mei 2020Ujumbe wa Uingereza kwenye Umoja wa Mataifa umetoa ombi hilo baada ya kikao cha ndani cha baraza la usalama la Umoja huo kutokana na kuongezeka kwa wasiwasi kuhusu mapigano baina ya majimbo hayo mawili kati ya vikosi vya serikali na jeshi la Arakan ambao ni wanamgambo waliojiimarisha wa msituni wanaowakilisha jamii ya wachache ya Budhaa wa jimbo la Rakhine.
Taarifa ya ujumbe huo imesema janga la virusi vya corona linawaweka raia walioko hatarini katika kitisho cha dharura cha kibinaadamu na hasa wakimbizi, watu walioyakimbia makaazi yao na jamii ya Waislamu walio wachache ya Rohingya wanaokabiliwa na vizuizi vya nyongeza.
Zaidi ya Warohingya 700,000 walikimbilia Bangladesh wakitokea Rakhine baada ya vikosi vya usalama vya Myanmar kuanzisha hatua kali mwezi Agosti mwaka 2917 kujibu shambulizi lililofanywa na kundi la waasi la Rohingya. Bangladesh inahifadhi zaidi ya wakimbizi milioni 1 wa Rohingya.
Baraza hilo la Usalama hata hivyo halikuarifu chochote baada ya kikao hicho, kufuatia taarifa fupi iliyosomwa na mjumbe maalumu wa Myanmar kwenye Umoja wa Mataifa Christine Schraner Burgener. Lakini wajumbe wanne wa Umoja wa Ulaya kwenye baraza hilo Estonia, Ubelgiji, Ufaransa na Ujerumani pamoja na mjumbe wa zamani Poland pia wameelezea wasiwasi wao kuhusu kusambaa kwa wanajeshi katika jimbo la Rakhine na Chin na kutoa mwito wa kusitishwa mara moja kwa mapigano kote nchini humo.
Wajumbe hao aidha wamesisitizia umuhimu wa jitihada za pamoja katika kushughulikia janga la COVID-19, zitakazolinda jamii zote na kuzingatia hatari inayowakabili wakimbizi walioko kwenye makambi ya Bangladesh pamoja na wakimbizi wa ndani.
Mwishoni mwa mwezi wa nne, mchunguzi kutoka shirika la haki ya binaadamu la Umoja wa Mataifa nchini Myanmar Yanghee Lee alitoa mwito wa kufanyika kwa uchunguzi mpya kuhusiana na madai na uhalifu dhidi a ubinaadamu wakati wa mapigano ya karibuni katika jimbo la rakhine na Chin. Alilituhumu jeshi la Myanmar kwa kusababisha mateso makubwa dhidi ya watu wa jamii ya walio wachache katika majimbo hayo mawili.
Ujumbe huo wa Uingereza umesema mzozo katika majimbo hayo umesababisha watu zaidi kuyakimbia makazi yao na kuzuiwa kupata misaada ya kiutu. Uingereza ilisema inatambua kwamba Myanmar inachukua hatua za kushughulikia janga la virusi vya corona, ikiwa ni pamoja na hatua za kupunguza kusambaa kwa maambukizi na imesema inaunga hatua hizo, lakini ikionya kuendelea kwa mzozo watu walio hatarini watakabiliwa na kitisho kikubwa zaidi kuliko sehemu nyingine yoyote.
Mashirika: APE