1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUfilipino

Ufilipino yaimarisha usalama kwenye viwanja vya ndege

6 Oktoba 2023

Ufilipino imeimarisha usalama katika viwanja vyake vya ndege Ijumaa hii baada ya mamlaka inayosimamia safari za anga kupata kitisho cha bomu kulipuliwa kwenye ndege za kibiashara.

https://p.dw.com/p/4XCw6
Rais wa Ufilipino Ferdinand Marcos Jr. akiwa na mgeni wake rais wa Hamlashauri kuu ya Ulaya, Ursula von der Leyen alipozuru nchini humo Julai 31, 2023. Oktoba 0, 2023, Ufilipino ilikabiliwa na kitisho cha kulipuliwa bomu kwenye ndege zake za biashara na kuimarisha usalama wa ndege hizo.
Rais wa Ufilipino Ferdinand Marcos Jr. akiwa na mgeni wake rais wa Hamlashauri kuu ya Ulaya, Ursula von der Leyen alipozuru nchini humo Julai 31, 2023. Oktoba 0, 2023, Ufilipino ilikabiliwa na kitisho cha kulipuliwa bomu kwenye ndege zake za biashara na kuimarisha usalama wa ndege hizo.Picha: Rolex dela Pena/Reuters

Mamlaka hiyo ya safari za anga nchini Ufilipino imesema inachunguza kitisho hicho walichopata kwa njia ya barua pepe na iliyotahadharisha kwamba kungetokea ‘mlipuko' wa ndege katika uwanja wa Manila na viwanja vingine vinne nchini humo.

Kutokana na kitisho hicho Mamlaka hiyo imesema usalama umeimarishwa katika jumla ya viwanja 42 kuanzia leo Oktoba 6 huku wakitumia pia mbwa wa kunusa.

Hakuna safari yoyote ya ndege iliyositishwa hadi sasa licha ya kitisho hicho na mamlaka kuimarisha hali ya usalama kwenye viwanja hivyo

Eric Apolonio, msemaji wa mamlaka hiyo ameliambia shirika la habari la AFP kwamba hadi sasa hakuna bomu ambalo limepatikana.