1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UgaidiMali

Kitisho cha ugaidi ni kikubwa Afrika, Afghanistan na Ulaya

Sylvia Mwehozi
2 Februari 2024

Ripoti iliyotolewa na jopo la wataalamu wa UN inasema kuwa kitisho cha ugaidi kutoka la Al-Qaeda, kundi la IS na washirika wake, kimesalia kuwa juu katika maeneo yenye mizozo barani Afrika na Afghanistan.

https://p.dw.com/p/4bxa6
Mwanajeshi wa Mali akishika bunduki aina ya AK-47
Mwanajeshi wa Mali akishika bunduki aina ya AK-47Picha: JOEL SAGET/AFP/Getty Images

Ripoti hiyo pia imebainisha ongezeko la ugaidi katika kanda nyingine ikiwa ni pamoja na Ulaya hasa kufuatia mashambulizi ya mwishoni mwa mwaka jana nchini Ufaransa na Ubelgiji.

Jopo la wataalam limesema katika ripoti hiyo yenye kurasa 23 kwamba utawala wa Taliban nchini Afghanistan bado una uhusiano wa karibu na kundi la Al-Qaeda.

Kanda ya Afrika Magharibi na Sahel pia imeshuhudia ongezeko la vurugu na vitisho huku serikali ya Somalia ikiendeleza mashambulizi dhidi ya kundi la Al-Shabaab ambalo bado lina nguvu.