1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kiwanda cha simu za Nokia Ujerumani kufungwa

22 Januari 2008
https://p.dw.com/p/Cw6c

BOCHUM:

Wafanya kazi wa kijerumani wamefanya maandamano mawili katika eneo la viwanda la Ruhr kupinga kufungwa kwa kiwanda cha kuunganisha simu za mknoni cha Nokia.Waandamanji wapatao elf 20 wamehudhuria maanamano yaliyoitishwa na chama cha wafanya kazi cha Ujeruamni.Nokia ilitangaza wiki jana kuwa inapanga kufunga kiwanda chao cha Bochum.Hii ina maana kuwa watumishi wake zaidi ya elf 2 watapoteza kazi zao.