Kiwango cha ukosefu wa ajira Afrika Kusini chaongezeka
15 Mei 2024Ofisi ya taifa ya takwimu imesema kiwango cha ukosefu wa ajira kimefikia asilimia 32.9 kati ya mwezi Januari na Machi, ongezeko hilo likiwa asilimia 0.8 tofauti ya kipindi kama hicho mwaka uliopita.
Ofisi hiyo ya takwimu imeendelea kueleza kuwa, idadi ya watu wasiokuwa na ajira iliongezeka kwa 330,000 hadi milioni 8.2.
Soma pia: Afrika Kusini yaadhimisha miaka 30 ya demokrasia
Ukosefu wa ajira ni moja kati ya masuala muhimu ya kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu Mei 29. Vijana wengi wanalalamikia ukosefu wa ajira katika taifa ambalo linachukuliwa kuwa lenye uchumi mkubwa zaidi barani Afrika.
Uungwaji mkono kwa chama tawala cha African National Congress (ANC), kilichokuwa madarakani tangu mwaka 1994, umepungua hadi chini ya asilimia 50 kabla ya uchaguzi mkuu kufanyika.