1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaKorea Kusini

K.Kusini na Marekani wajadili mazoezi ya pamoja ya nyuklia

3 Januari 2023

Korea Kusini na Marekani zinajadili uwezekano wa mazoezi ya pamoja wakitumia zana za Marekani.

https://p.dw.com/p/4LfqU
Südkorea Militär-Übung
Picha: South Korean Defence Ministry/AFP

Korea Kusini na Marekani zinajadili uwezekano  wa mazoezi ya pamoja wakitumia zana za Marekani.Hayo yamewekwa wazi na  Rais wa Korea Kusini Yoon Suk-yeol huku kiongozi wa Korea Kaskazini akitaja Korea Kusini ni "adui asiye na shaka" katika mvutano.

Rais Yoon katika mahojiano yake  yaliochapishwa katika gazeti yalifatiwa na wito wake wa maandalizi  ya vita kwa uwezo mkubwa  baada ya mwaka ulioshuhudia majaribio ya idadi ya makombora ya Korea Kaskazini na uvamizi wake iliofanya wiki iliopita kwa kutumia ndege zisizokuwa na rudani.

Ikulu ya White House na wizara ya mambo ya nje ya Marekani hazikutoa kauli kuhusiana matamshi ya Yoon, na msemaji wa Pentagon amesema leo kuwa hawana cha kutangaza.