Kocha wa Gladbach apatikana na Covid
9 Machi 2022Makamu wake Christian Peintinger atasimamia pambano la Jumamosi (12.03.2022) dhidi ya Hertha baada ye Huetter na maafisa wawili wa timu yake ya ukufunzi kupatakiana na ugonjwa huo.
Mechi ya Jumamosi ina umuhimu mkubwa wa ziada kwa kocha huyo raia wa Austria, ambaye anakabiliwa na shikizo, huku Gladbach wakielea juu ya nafasi za kushuka daraja baada ya kupoteza mechi ya wikendi iliyopita 3-2 dhidi ya Stuttgart licha ya kuongoza kwa mabao mawili.
Kupoteza ugenini lilikuwa pigo lingine kwa timu ya Gladbach ambayo ina "vitu elfu moja kuvifanyia kazi" kwa mujibu wa mshindi wao wa kombe la dunia 2014 Christoph Krammer.
Kama Huetter, kocha wa Hertha Berlin, Tayfun Korkut, yuko chini ya shinikizo baada ya kisago cha 4-1 wikendi iliyopita kutoka kwa Eintracht Frankfurt kilichoisukuma timu hiyo ya mji mkuu Berlin katika nafasi ya 16.
Ongezeko la idadi ya visa vya maambukizi ya Covid nchini Ujerumani limeathiri pia timu nyingine za Bundesliga. Mainz inataka kuwasilisha ombi la kutaka mechi yake ya Jumamosi dhidi ya Augsburg ichezwe tarehe nyingine baada ya wikendi iliyopita mechi yao dhidi ya Borussia Dortmund kuahirishwa hadi Machi 16 kwa sababu ya visa 20 vya maambukizi katika kikosi chao.
Baadhi ya wachezaji wa Mainz huenda wakawa tayari kucheza tena kufikia wikendi, lakini sehemu kubwa ya wachezaji yumkini wakalazimika kwenda moja kwa moja kwenye basi la timu kutokea karantini," alionya mkurugenzi Christian Heidel.
Timu nyingine pia zimeathirika hivyo hivyo. Siku ya Jumanne, Borussia Dortmund ilithibitisha mabeki Mats Hummels na Raphael Guerreiro wote wamepatikana na Covid. Pia, timu ya wakufunzi ya Arminia Bielefeld wameathiriwa, hali ambayo huenda ikaathiri mechi ya Jumamosi.
(AFP)