Kombe la Afrika hatima ya Nigeria ?
25 Januari 2008Katika changamoto za jana za kombe la Afrika la mataifa,mabingwa mara 4-Ghana walitia mguu mmoja katika robo-finali ya kombe hilo baada ya kuizaba bao 1:0 Namibia iliofufuka kutoka pigo kali ililopata kwa Morocco la mabao 5-1.
Kabla Ghana na Namibia, Guinea ilichukua pointi 3 kutoka Morocco na kuepuka kufunga virago na mapema kwa safari ya Conackry.Guinea,kwahivyo imelipiza kisasi cha kulazwa na simba hao wa Atlas katika finali ya kombe la Afrika 1976 mjini Addis Ababa.
Mabingwa mara 2-Nigeria wakiongozwa na kocha wa zamani wa taifa wa Ujerumani Berti Vogts huenda leo wakafugishwa virago na kurudi Abuja, ikiwa watashindwa kutamba mbele ya Mali.
Kwa Super Eagles-Nigeria,leo ni kufa-kupona lakini pia kwa kocha wao mjerumani Berti Vogts.Kwani, ikiwa Mali itaitimua nje Nigeria leo,basi Super eagles –timu ilio kileleni kabisa mwa orodha ya FIFA ya timu bora kuliko yoyote ya Afrika,haina budi kurudi nyumbani.Nyumbani pia huenda akarudishwa kocha wao Berti Vogts ambae ataonekana kwamba baada ya kushindwa kufua dafu na Scotland pia hana lake jambo kwa Nigeria.Berti anaelewa hayo. Anasema, „Wachezaji wangu wana ari kubwa ya kitimu na najua watajitolea wawezavyo ili kuingia duru ijayo.“Asema Vogts.
Nigeria imewasili nusu-finali ya kila kombe la dunia tangu 2000. Nigeria ilizabwa bao 1:0 na Tembo wa ivory Coast katika mpambano wao wa kwanza .
Mpambano wapili leo utakua kati ya Benin na Tembo wa Corte d’ Iviore inayotaka kufuata nyao za wenyi Ghana kushinda mpambano wao wapili.
Mahasimu wao leo ni Benin, ambayo kocha wao mjerumani Reinhard Fabisch amefichua hivi punde kwamba mtu mmoja aliejiita Andrews alimuendea hotelini kwake kabla ya mpambano kati ya Benin na Mali na kutaka kumpa mrungura wa kitita cha dala 20,000 ikiwa ataiachia Mali ishinde.Alimjibu atokomee haraka au angeita polisi.“Mtu huyo alidai anawafanyia kazi watu fulani barani Asia ambao wako tayari kulipa kitita hicho.Hatahivyo, Benin ilishindwa na Mali kwa bao 1:0.
Mabingwa mara 4 Ghana wana nusu ya tiketi ya duru ijayo ya robo finali baada ya jana kuitoa namibia kwa bao 1:0. Stadi wa Nottingham Forest Junior Agogo,aliufumania mlango wa namibia tayari katika kipindi cha kwanza na kwa ushindi huo ,Black Stzars-Ghana, wameparamia kilelelni mwa kundi hili A.Sasa Ghana i ina miadi na Morocco katika mpam,bano wao wa mwisho wa duru hii ya kwanza.Kwa morocco iliozabwa mabao 3-2 na Guinea jana, itakua kufa-kupona.Ghana,itahitaji alao pointi moja kutoka Morocco kuhakikisha Kombe la 26 la Afrika halimalizikii duru ya kwanza kwa mashabiki wa Ghana.
Morocco kwa upande wake baada ya kuirarua namibia kwa mabao 5-1, inajua kwamba bila ushindi dhidi ya Ghana,Guinea na Ghana zitasonga mbele na kuwaacha simba wa Atlas wananguruma katika milima yao ya Atlas.
Namibia sasa ina miadi na Guinea ambayo baada ya kutia mfukoni pointi 3 jana,itachachamaa kweli kunyakua pointi 3 nyengine kutoka Namibia na kuwaachia wenyeji Ghana na Morocco kumalizana wenyewe kwa wenyewe.