Kompany achaguliwa kuwa kocha ajaye wa Bayern: Rummenigge
29 Mei 2024Mwanachama wa bodi ya klabu hiyo Karl-Heinz Rummenige amesema mkurugenzi wa spoti wa klabu ya Bayern Munich Max Erbel amemchagua Kompany kuwa kocha mpya.
Rummenige, ambaye ni mshambuliaji wa zamani wa Bayern Munich mwenye umri wa miaka 68 ameiambia televisheni ya Sky Italia kuwa kocha wa Manchester City Pep Guardiola aliwasaidia katika chaguo lao. Kompany ana uzoefu wa Bundesliga, baada ya kuichezea Hamburg kabla ya kujiunga na Man City.
Soma pia: Julian Nagelsmann anatakiwa Bayern Munich kumrithi Tuchel
Alichukua mikoba katika klabu ya Burnley mwaka wa 2022, na kuwapandisha katika Ligi Kuu ya England baada ya kuibuka mabingwa wa daraja la pili msimu huo. Hata hivyo, klabu hiyo ilishuka daraja baada ya msimu mmoja katika Ligi ya Premier. Kompany ndiye mgombea wa karibuni kabisa kwenye orodha ndefu ya makocha waliohusishwa na Bayern.