1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kongamano la kiinjili mjini Cologne

Oummilkheir6 Juni 2007

"Wamedhamiria kujenga daraja kuwaunganisha jamii" anasema mwenyekiti wa kongamano la kinjili

https://p.dw.com/p/CHkf
Picha: AP

Kongamano la 31 la kanisa la kiinjili la Ujerumani limeanza hii leo mjini Cologne.Kila baada ya miaka miwili wakristo wanachanganyika ili kusherehekea kwa pamoja , kuabudu na akupashana habari kuhusu masuala tofauti.Masuala hayo hayahusiani pekee na dini.Hata masuala ya kijamii na masuala mengineyo yanajadiliwa.

Zaidi ya waumini laki moja wa ndani na maelfu ya wageni wanahudhuria kongamano hili la jadi katika jiji la Cologne.Maonyesho zaidi ya elfu tatu pamoja na mijadala ni miongoni mwa vivutio vya kongamano hilo lililopewa jina safari hii:”Kwa uchangamfu,kwa nguvu na vikali”-pakiwepo pia sherehe mbali mbali,burudani na vitumbuizo vyenginevyo.

Kivutio kikubwa zaidi lakini katika kongamano hili la kanisa la kiinjili ,mbali na ibada ni mijadala kuhusu masuala moto moto ya wakati huu tulio nao.Kongamano la mwaka huu linatazamiwa kugubikwa na mada zile zile zinazojadiliwa katika mkutano wa viongozi wa mataifa tajiri kiviwanda G-8 mjini Heiligendamm.

Akizungumza na kituo cha matangazo cha Deutschland Radio,mkuu wa kanisa la kiinjili katika jimbo la mto Rhine NIKOLAUS SCHNEIDER alisema:

“Nnataraji mwito wetu utasikilizwa pia na viongozi mjini Heiligendamm.Kwa jinsi gani mwito huu unaweza kushawioshi majadiliano,siwezi kuashiria.Lakini nnaamini watausikia na nnaamini kuna watu pia wanaotaka kujua nini kitasemwa kutoka Cologne.”

Kwa upande wake mwenyekiti wa kongamano hili la kanisa la kiinjili Reinhard Höppner anasema lengo lao ni kujenga daraja na kupunguza mivutano miongoni mwa jamii.Hali ya uchumi ulimwenguni,Afrika, kuhifadhiwa hali ya hewa pamoja na mizozo ya mashariki ya kati itajadiliwa pia katika kongamano hilo litakaloendelea hadi June 10 ijayo.

“Tutajenga daraja zaidi ili kuwajongeza walio ndani na wale walio nje ya senyenge” amesema mkuu wa kanisa la kiinjili nchini Ujerumani Reinhard Höppner.

Mada nyengine muhimu ni kuhusu midahalo kati ya waumini wa dini tofauti.