1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAngola

Kongo na Rwanda zasisitiza haja ya kuheshimu usitishaji vita

6 Novemba 2024

Mawaziri wa mambo ya nje wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Rwanda wamethibitisha haja ya pande zinazozozana kuheshimu makubaliano ya usitishaji mapigano mashariki mwa Kongo.

https://p.dw.com/p/4mfHv
Rais wa Rwanda Paul Kagame (kushoto) Rais wa Angola Joao Lourenco (katikati) na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Felix Tshisekedi ( kulia) walipokutana mjini Luanda Angola mnamo Julai 6, 2022 kwa mazungumzo baada ya kuongezeka kwa ghasia mashariki mwa Kongo
Rais wa Rwanda Paul Kagame (kushoto) Rais wa Angola Joao Lourenco (katikati) na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Felix Tshisekedi ( kulia)Picha: JORGE NSIMBA/AFP

Waakilishi wa Kongo na Rwanda walikutana na waziri wa mambo ya nje wa Angola Tete Antonio mjini Goma katika jimbo la Kivu Kaskazini, mashariki mwa Kongo, karibu na mpaka kati ya Kongo na Rwanda kuzindua kamati ya kufuatilia ukiukaji wa makubaliano ya kusitishwa kwa vita.

Angola kuongoza juhudi za upatanishi kati ya Rwanda na DRC

Baada ya mkutano huo, Antonio aliwaambia waandishi wa habari kwamba wote walisisitiza kuhusu haja ya kuheshimu makubaliano hayo na kuongeza kuwa njia ya sawa ni kupatikana kwa amani.

Rwanda yasema bado iko katika mchakato wa kutafuta amani

Kwa upande wake, waziri wa mambo ya nje wa Kongo Therese Kayikwamba Wagner, hakutoa tamko lolote baada ya mkutano huo.

Waziri wa mambo ya nje wa Rwanda Olivier Nduhungirehe, alisema nchi yake bado iko katika mchakato wa kutafutaamani.

Kamati hiyo ya kufuatilia usitisahji wa mapigano itaongozwa na Angola na kujumuisha waakilishi wa Kongo na Rwanda.