1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaKorea Kusini

Korea kaskazini iko tayari kuishambulia Korea Kusini

14 Oktoba 2024

Korea Kaskazini imesema Jumapili kuwa vikosi vyake vya kijeshi viko tayari kuanzisha mashambulizi dhidi ya Korea Kusini, hatua ambayo imeongeza shinikizo kwa taifa hilo pinzani.

https://p.dw.com/p/4ljz1
Kiongozi wa Korea Kaskazini - Kim Jong Un akitoa hotuba katika chuo kikuu cha ulinzi wa taifa cha Kim Jong Unmnamo Oktoba 7 2024, mjini Pyongyang, wakati wa maadhimisho  ya miaka 60 tangu kuanzishwa kwake
Kiongozi wa Korea Kaskazini - Kim Jong Un Picha: KCNA VIA KNS/AFP

Korea Kusini imekataa kuthibitisha iwapo ilituma droni hizo lakini ikaonya kuwa itaiadhibu vikali Korea Kaskazini ikiwa usalama wa raia wake utatishiwa.

Siku ya Ijumaa, Korea Kaskazini iliishutumu Korea Kusini kwa kurusha karatasi hizo kwa mara ya tatu mwezi huu na kutishia kuwa itajibu vikali ikiwa tukio hilo litajirudia tena.

Soma pia:Korea Kaskazini yaimarisha uwezo wa silaha zake za nyuklia

Katika taarifa iliyotolewa na vyombo vya habari vya serikali ya Korea Kaskazini hapo jana, wizara ya ulinzi ya nchi hiyo imesema kuwa jeshi lake lilitoa agizo la awali kwa vitengo vya kijeshi vya silaha pamoja na vingine karibu na mpaka na Korea Kusini kujiandaa kikamilifu kwa mashambulizi.