SiasaKorea Kaskazini
Korea Kaskazini kurusha satelaiti 3 mwaka 2024
31 Desemba 2023Matangazo
Uamuzi wa kurushwa kwa satelaiti hizo za ujasusi ulitangazwa katika mkutano wa chama tawala na kuwa moja ya uamuzi muhimu wa kisera kwa mwaka 2024, limesema shirika la habari la serikali, KNCA.
Mkutano huo wa siku tano ulihudhuriwa pia na kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un.
Kim aidha, alitangaza mipango ya kutengeza ndege zisizo na rubani, kuendeleza uwezo wa vita vya kielektroniki, pamoja na kuimarisha nguvu za nyuklia na makombora.
Mwaka 2023, Taifa hilo lilivunja rekodi ya majaribio ya silaha na inalenga kuongeza uwezo wake wa kijeshi, huku Japan, Korea Kusini na Washington wakiimarisha ushirikiano unaolenga kuikabili mikakati hiyo ya Pyongyang.