1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Korea kaskazini kuwekewa vikwazo zaidi.

11 Juni 2009

Kura ya kupitisha azimio la baraza la usalama la umoja wa mataifa la kuiwekea vikwazo Korea Kaskazini, itafanyika hapo kesho.

https://p.dw.com/p/I7Oe
Kiongizi wa Korea Kaskazini Kim Jong IlPicha: picture-alliance/ dpa

Umoja wa mataifa umechukua hatua za kuiwekea vikwazo zaidi Korea kaskazini baada ya taifa hilo la kikoministi kulifanyia jaribio kombora huku pia likiwa kwenye mazungumzo na jirani yake korea kusini, kuhusu kiwanda kinachokakabiliwa na matatizo.

Azimio hilo la bazara la usalama la umoja wa mataifa lilioandandikwa na Marekani na kuungwa mkono na wanachama wengine wa wanne wa kudumu wa umoja wa mataifa pia Japan na Koresa kusini ambalo litapigiwa kura kesho ijumaa, huenda likawa pigo kwa shughuli za kibiashara kupitia usafiri wa baharini kwa Korea kaskazini.

Inaaminika kuwa hatua hiyo huenda ikafanya Korea kaskazini kuchukua hatua zaidi ikiwa azimio hilo litapitishwa baada ya kutishia kuwa, italifanyia jaribio kombora la masafa marefu, ikiwa baraza la usalama la umoja mwa mataifa halitaiomba msamaha kutoka na adhabu dhidi yake kufuatia hatua za korea kaskazini za kurusha roketi angani mwezi Aprili mwaka huu, kitu ambacho kilionekana kama jaribio la kombora la masafa marefu.

Ikiwa azimio hili litapitishwa na baraza la usalama la umoja wa mataifa,litakuwa kali, na litakuwa kali kwa njia inayofaa, alisema Susan Rice, balozi wa Marekani katika umoja wa mataifa.

Korea kaskazini imewekewa vikwazo kwa miaka kadha kutokana na shughuli zake za kijeshi ambazo zinapingwa na mataifa ya eneo hilo.Hata hivyo wadadisi hawana uhakika ikiwa vikwazo hivyo vipya vitakuwa vya maana katika taifa hilo ambalo linaendelea kuzoroteka kiuchumi tangu kiongozi wake Kim Jong Il aingie madarakani mwaka 1994.

Azimio hilo linalaani vikali jaribio la kinyuklia lililofanywa na Korea kaskazini mwezi uliopita, na kuitaka isifanye jaribio kama hilo kwa kutumia teknolojia ya makombora yanayoweza kurushwa kutoka kwa bara moja hadi lingine.

Nordkorea Kurzstreckenrakete Test
Kombora larushwa angani nchini Korea Kaskazini.Picha: AP

China na Urusi zimekuwa zikipinga azimio za hapo awali za kuzitaka nchi zote kuzifanyia ukaguzi meli za Korea kaskazini, ambazo zinakisiwa kubeba mizigo ambayo inaweza kukiuka vikwazo vya kibiashara na silaha vilivyowekwa na umoja wa mataifa.

Kwenye mfumo wa sasa wa azimio hilo umoja wa mataifa, unatoa wito kwa mataifa kukagua mizigo baharini angani na kwenye ardhi, lakini haishinikizi azimio lenyewe. Biashara ya silaha ni kati moja ya tegemeo za kifedha za Korea kaskazini.

China, mshirika wa karibu wa korea kaskazini huenda isikubali vikwazo hivyo vipya ambavyo vitataziza shughuli zake za kiuchumi na Korea kaskazini au ambavyo pia vinaweza kusambaratisha kabisa uchumi wa nchi hiyo ambao kwa sasa uko katika hali mbaya.

Hata hivyo China kwa upande mwingine haioni maana ya kupinga azimio hili kwa kwa kuwa haijanufaika kwa vyo vyote vile, alisema Shi Yinhong mtaalam katika chuo kimoja nchini china akielezea ni kwa nini china inaonekana kulegeza msimamo wake.

Korea kaskazini imeyakasirisha mataifa katika eneo hilo na nchi zingine za mbali kwa muda wa wiki chache zilizopita, kutokana na hatua zake za kuendesha majaribio ya kijnyuklia, suala ambalo lilizifanya Marekani na korea kusini kuweka vikosi vyake katika tahdahari ya juu tangu vita kati ya korea kaskazini na kusini kati ya mwaka 1950-1953.

Maafisa nchini Korea kusini wanasema kuwa Korea kaskazini inaandaaa kulifanyia jaribio kombora la masafa marefu ambalo lina uwezo wa kufika nchini marekani na kombora lingine la masafa ya kati ambalo linaweza kufika nchini korea kusini na Japan.

Mwandishi :Jason Nyakundi/RTR

Mhariri :Mohammed Abdul Rahman