1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Korea Kaskazini yaapa kuimarisha ushirikiano na China

29 Julai 2023

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un, amekutana na wajumbe wa China waliotembelea nchi hiyo kwa sherehe za kumbukumbu ya miaka 70 ya kumalizika kwa Vita vya Korea na kuapa kuendeleza uhusiano wa nchi hizo mbili.

https://p.dw.com/p/4UX5z
Kim Jong Un katika maadhimisho ya miaka 70 ya kumalizika kwa vita vya Korea
Kim Jong Un katika maadhimisho ya miaka 70 ya kumalizika kwa vita vya KoreaPicha: KCNA/REUTERS

Haya yameripotiwa leo na shirika la habari la serikali ya Korea Kaskazini, KCNA. Kim aliwapokea maafisa hao wa China wakiongozwa na mwanachama wa kamati ya sera ya chama cha kikomunsiti Li Hongzhong hapo jana. Ujumbe huo wa China ni wa kwanza tangu kuzuka kwa janga la Uviko 19.

Soma zaidi: Kim Jong Un akutana na wajumbe kutoka Urusi na China

KCNA imeripoti kuwa kilichosisitizwa katika mazungumzo hayo ni msimamo wa vyama na serikali za mataifa hayo mawili kukabiliana na hali ngumu ya kimataifa kwa hiari yao wenyewe na kuimarisha kwa uthabiti urafiki na ushirikiano kwa kiwango kipya cha hali ya juu.