1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Korea Kaskazini yafyatua makombora ya masafa marefu

1 Julai 2024

Jeshi la Korea Kusini limesema kuwa Korea Kaskazini hii leo imefyatua makombora mawili ya masafa, ikiwa ni hatua ya hivi karibuni katika msururu wa majaribio ya silaha yanayofanywa na Pyongyang.

https://p.dw.com/p/4hhuV
Korea Kaskazini
Kombora la masafa marefu la Korea KaskaziniPicha: Korean Central News Agency/AP/picture alliance

Jeshi la Korea Kusini limesema kuwa Korea Kaskazini hii leo imefyatua makombora mawili ya masafa, ikiwa ni hatua ya hivi karibuni katika msururu wa majaribio ya silahayanayofanywa na Pyongyang.

Kwa mujibu wa jeshi la Korea Kusini, kombora la kwanza la masafa ya kati lilifyatuliwa majira ya asubuhi leo Jumatatu na kufuatiwa na jingine dakika 10 baadae, ambalo halijatambulika.

Uhusiano baina ya nchi hizo mbili umefikia kiwango cha chini kabisa, huku Pyongyang ikizidisha majaribio yake ya silaha na kutuma maputo ya takataka dhidi ya jirani yake Seoul.

Pyongyang tayari ilirusha maelfu ya maputo yenye takataka katika kile ilichoita ni kulipizia kisasi hatua ya Korea Kusini ya kurusha maputo yaliyokuwa na karatasi zilizoandikwa propaganda za kuipinga serikali ya Korea Kaskazini.