1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaKorea Kaskazini

Korea Kaskazini yafyatua makombora ya masafa mafupi

23 Desemba 2022

Jeshi la Korea Kusini limesema kuwa Korea Kaskazini leo imefyatua makombora mawili ya masafa mafupi kuelekea katika bahari ya mashariki.

https://p.dw.com/p/4LMfN
Taiwan Militärübung
Picha: Chiang Ying-ying/AP/picture alliance

Makombora hayo yametumwa siku chache baada ya ndege za kivita za Marekani na Korea Kusini kufanya luteka ya pamoja katika hatua ambayo Korea Kaskazini inaiona kama mazoezi ya uvamizi.

Jeshi la Korea Kusini limegundua ufyatuaji huo wa makombora majira ya saa kumi na nusu jioni kwa saa za Asia Mashariki.

Siku ya Jumanne, ndege za kivita zenye uwezo wa kuwa na nyuklia za Marekani ziliruka katika Rasi ya Korea katika luteka ya pamoja na ndege za kivita za Korea Kusini.

Wizara ya Ulinzi ya Korea Kusini imesema luteka hiyo ilikuwa sehemu ya makubaliano ya pande hizo mbili katika kuimarisha dhamira ya Marekani ya kumlinda mshirika wake wa Asia kwa uwezekano wowote wa kijeshi, ikiwemo nyuklia.