SiasaAsia
Korea Kaskazini yaikosowa Marekani kuipa silaha Ukraine
11 Julai 2023Matangazo
Waziri wa Mambo ya Nje wa Korea Kaskazini Choe Son Hui amesema katika taarifa iliyochapishwa na shirika la habari la Korea kuwa "Marekani imefanya chaguo hatari kwa kutoa silaha kwa Ukraine."
Wiki iliyopita, Washington ilitangaza kuipa Ukraine silaha zilizopigwa marufuku kwa ajili ya kujilinda dhidi ya uvamizi wa Urusi.
Soma zaidi: Biden awasili Uingereza kabla ya mkutano wa NATO
Bi Choe ameeleza kuwa hatua ya Marekani inaonesha kwa mara nyengine namna Marekani ilivyo mharibifu wa amani na kuchukua sifa za uchokozi na mauaji kama sera yake ya kimataifa.
Hata hivyo, katika ukosoaji wake huo, hakuzungumzia juu ya madai dhidi ya Urusi ya kutumia silaha zilizopigwa marufuku katika vita vyake nchini Ukraine.