1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Korea Kaskazini yakosoa kauli ya G7 kuhusu nyuklia yake

Sylvia Mwehozi
14 Novemba 2023

Korea Kaskazini imekosoa kauli ya pamoja iliyotolewa na mawaziri wa mambo ya nje wa nchi zilizopiga hatua kiviwanda za G7, ya kukosoa mpango wa nyuklia wa nchi hiyo.

https://p.dw.com/p/4Ym65
Korea Kaskazini | Gwaride la kijeshi mjini Pyongyang
Gwaride la kijeshi la Korea KaskaziniPicha: Yonhap/picture alliance

Afisa wa ngazi ya juu katika wizara ya mambo ya nje ya Korea KaskaziniJo Chol Su, amesema kundi hilo la nchi tajiri linapaswa kuvunjwa mara moja.

Wiki iliyopita, wanadiplomasia wakuu wa G7 walisisitiza wito wao wa muda mrefu wa kuondolewa kabisa kwa silaha za nyuklia katika Rasi ya Korea. Mawaziri hao pia waliitaka Pyongyang kuachana na silaha zake za nyuklia.

Soma pia: Korea Kaskazini yavurumisha makombora mengine ya masafa

Katika taarifa ya pamoja, wanadiplomasia hao walilaani hatua ya Pyongyang ya kuipatia silaha Urusi, wakizitaka nchi hizo mbili kusimamisha mara moja shughuli zote hizo.

Korea Kaskazini imekataa madai hayo na kulaani taarifa ya G7 iliyoitaja kuwa haina msingi.