1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Korea Kaskazini yarusha makombora kabla ya Trump kurejea

14 Januari 2025

Korea Kusini imesema Korea Kaskazini imefyatua makombora kadhaa ya masafa mafupi kuelekea baharini, tukio lililoripotiwa na jeshi lake, likijiri kabla ya kurejea kwa Trump.

https://p.dw.com/p/4p8Jr
Televisheni ya Korea Kusini: Korea Kaskazini yarusha makombora ya masafa mafupi
Televisheni ya Korea Kusini: Korea Kaskazini yarusha makombora ya masafa mafupi.Picha: Kim Jae-Hwan/SOPA/picture alliance

Majaribio hayo yamejiri wakati Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan Takeshi Iwaya akiwa ziarani Korea Kusini kwa mfululizo wa mikutano na maafisa waandamizi, huku majirani zake hao wa Asia wakitaka kuimarisha uhusiano baina ya nchi hizo kabla ya rais wa Marekani Donald Trump kuingia madarakani wiki ijayo.

Soma pia:Korea Kaskazini yafanya majaribio ya makombora mapya ya masafa mafupi 

Jeshi la Seoul limesema liligundua makombora kadhaa ya masafa mafupi yaliyofyatuliwa kuelekea Bahari ya Mashariki. Kaimu rais wa Korea Kusini Choi Sang-mok amekemea urushaji huo wa makombora, akisema unakiuka maazimio ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Amesema Seoul itajibu vikali vitendo vya uchokozi vinavyofanywa na Korea Kaskazini kwa kuzingatia uwezo wake thabiti wa usalama na ushirikiano na Marekani. Watalaamu wanasema urushaji huo wa karibuni huenda unanuia kutuma ujumbe kwa utawala unaokuja wa Trump.