Korea Kaskazini yashutumu nchi za Magharibi kwa kuichunguza
13 Mei 2024Kulingana na shirika la habari la serikali KCNA, Korea Kaskazini imesema itachukua hatua muhimu ili kulinda uhuru na usalama wake.
Pyongyang imezitaka Uingereza, Canada, Ujerumani, Ufaransa, New Zealand na Australia kuacha mara moja kile walichokiita "uingiliaji wao wa kijeshi" katika eneo la Asia-Pacific kwa kutumia vikwazo vya Umoja wa Mataifa kama kisingizio.
Korea Kusini na Uingereza zilifanya doria za pamoja baharini karibu na rasi ya Korea mnamo mwezi Aprili ili kutekeleza vikwazo vya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa dhidi ya Korea Kaskazini.
Soma pia: Korea Kaskazini ilipeleka makontena 7,000 ya silaha Urusi
Wakati huo huo, Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un ametembelea kiwanda cha silaha na kukagua silaha kama vile bunduki za sniper na maroketi.
Akiwa ameandamana na viongozi wa ngazi ya juu katika serikali yake, Kim alisifu ubora wa silaha hizo na kuvitaka viwanda hivyo kutekeleza mipango ya utengenezaji silaha bila kukosa.