Korea Kusini haijajibiwa juu ya msaada kwa Korea Kaskazini
2 Agosti 2024Naibu msemaji wa wizara ya muungano ya Korea Kusini, Kim In-ae, amewaambia waandishi wa habari kuwa Korea Kaskazini iko tayari kutoa msaada wa dharura wa kiutu kwa wahanga wa mafuriko hayo. Mapema wiki hii, Korea Kaskazini ilisema mvua kubwa ambazo hazijawahi kushuhudiwa nchini humo zilinyesha katika eneo la mpaka wake wa kaskazini karibu na China, na kusababisha mzozo mkubwa ambapo zaidi ya watu elfu 5 walitengwa katika eneo hilo ambalo hukumbwa na mafuriko mara kwa mara. Kituo cha kitaifa cha habari Korea Kaskazini kiliripoti juzi Jumatano kuwa kiongozi wa nchi hiyo Kim Jong Un ameahidi kuwaadhibu vikali maafisa waliozembea katika majukumu yao ya kuzuia majanga na kusababisha vifo vya watu. Ripoti moja ya kituo cha televisheni cha Korea Kusini TV Chosun, imesema kuwa mamia ya watu wamefariki dunia.