MigogoroKorea Kusini
Korea Kusini yaituhumu Pyong Yang kupeleka wanajeshi Urusi
18 Oktoba 2024Matangazo
Shirika la kijasusi la nchi hiyo pia limesema kwamba Korea Kaskazini inashiriki katika vita vya Ukraine na imeamua kuwapeleka wanajeshi wapatao 12,000, nchini Urusi kikiwemo kikosi maalum cha wanajeshi. Hayo ni kwa mujibu wa shirika la habari la Korea Kusini, Yonhap.
Rais wa Korea Kusini Yoon Suk Yeol ameitisha mkutano wa usalama wa dharura na maafisa wakuu wa kijasusi, jeshi na wa usalama wa taifa kujadili kuhusika kwa wanajeshi wa Korea Kaskazini katika vita vya Urusi dhidi ya Ukraine. Urusi na Korea Kaskazini zote zimekanusha madai hayo.
Ikulu ya Urusi imesema madai hayo ya kupelekwa majeshi ya Korea Kaskazini nchini mwake ili kuisadia katika vita vyake dhidi ya Ukraine sio ya kweli.